Depay akatwa kikosini


Huenda huu ndio ukawa  mwisho wa mchezaji Memphis Depay katika timu ya manchester united baada ya kukatwa kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza fainali ya kombe la FA leo.

Depay ameshindwa kuonesha makali yake tangu ajiunge na mashatani hao wa jiji la Manchester na huenda timu hiyo ikaachana naye.

Licha ya kufanya vizuri na kuwa mfungaji bora akiwa na timu ya PSV nchini uholanzi lakini ameshindwa kufanya vitu vya ziada katika timu hiyo na anaonekana hana msaada.



Depay atakosa fainali ya leo itakayochezwa Wembley dhidi ya Crystal Palace baada ya kutojumuishwa kabisa kwenye timu hadi katika upande wa wachezaji wa akiba.

Dalili zinaonesha huenda Manchester united ikaachana na mchezaji huyo kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi 2016/17.

Comments