Kiungo wa timu ya Leicester city Danny Drinkwater ameitwa rasmi kwenye timu ya Uingereza itakayoshiriki michuano ya Euro 2016 mwaka huu nchini Ufaransa.
Drinkwater 26, anaweka historia baada ya kuitwa kwa mara ya kwanza kwenye timu ya taifa Uingereza baada ya kunyakua ubingwa na timu ya Leicester city.
Mchezaji huyo aliyechipukia katika timu ya Manchester united amekuwa nguzo katika timu ya Leicester akiwa na ufanisi mkubwa wa kukaba katika sehemu ya katikati na juhudi zake zimezaa ubingwa kwa timu hiyo ambayo imetwaa ubingwa England chini ya Claudio Ranieri
Wengine walioitwa ni
Jordan Henderson, Jack wilshere, Andros Townsend, James Milner, Eric Dier, Adam Lallana, Wayne Rooney, Marcus Rashford, Daniel Sturridge, Jamie Vardy, Harry Kane, Ryan Betrand, Danny Rose, Chris Smalling, John stones, Gary Cahil, kyle Walker na Nathaniel Clyne.

Comments
Post a Comment