Timu ya Liverpool sasa haitaki masihara baada ya timu hiyo kuwa kwenye wakati mzuri wa kukamlisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Mario Gotze.
Liverpool imeweka mezani dau la euro 20 milioni ili kuhakikisha mchezaji anatua kwenye timu hiyo na kuongeza nguvu kwenye kikosi cha sasa.
Kocha wa liverpool Jurgen Klopp anaona Gotze ni mchezaji sahihi katika mapambano ya vita ubingwa mwaka dhidi ya Antinio Conte anayetua Chelsea, Pep Gurdiola Manchester city, Arsene Wenger Arsenal, Mauricio Pochettino Spurs na Jose Mourinho kama atatua old traffor..
Gotze 23, ni chimbuko la kocha Jurgen Klopp ambaye alimtumia sana alipokuwa akiinoa Borrusia Dortmund hivyo kuna uwezekano mkubwa dili la mchezaji huyo likatiki hivi karibu.
Gotze amekuwa hana namba ya kudumu tangu ajiunge na Bayern Munich hivyo milango ipo wazi kwa Liverpool.

Comments
Post a Comment