Kocha wa Manchester city Pep Gurdiola anakaribia kukamilisha dili la kumsajili kiungo wa Ujermani Ilkay Gundogan.
Vyanzo vya habari kutokana nchini Ujermani vimeripoti kuwa Mancity ilipeleka ofa ya awali ya euro 17.5 milioni lakini huenda dili hilo likafikia euro 20.1 milioni ili kukamilika kwa usajili wa mchezaji huyo.
Gundogan ambaye ataikosa michuano ya UEFA Euro Juni mwaka huu dili lake linaenda vizuri na huenda akasaini Man city siku za hivi karibuni.
Licha ya majeraha ya mara kwa mara lakini Gurdiola ana imani na mchezaji wakati huu akihitaji kuijenga City ambayo itakua chini yake msimu ujao.

Comments
Post a Comment