Hazard atimiza ahadi yake kuinyonga spurs


Mchezaji wa chelsea Edeni Hazard alifuta rasmi matumaini ya ubingwa kwa timu ya Tottenham Hotspurs baada ya kufunga bao la kuchomoa akitokea benchi.

Hazard alifunga bao hilo katika dakika ya 83 baada ya kupokea mpira kwa Diego Costa na kuzamisha wavuni bao hilo ambalo lilitkata tiketi ya kuwatawaza Leicester city kuwa mabingwa rasmi wa msimu wa EPL 2015/16.

Hazard ambaye hakuwa vizuri msimu huu alikaliliwa katika mitandao ya kijamii akisema kuwa hawatakubali timu nyingine ya London ichukue ubingwa huu, na badala watapigana kwa hali na mali kuhakikisha Leicester inabeba ubingwa huo.

Kwa kufunga bao hilo Eden Hazard ametimiza ahadi yake na kwa kuiwezesha Leicester city kuwa mabingwa kutokana na kuyafanya matokoe ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika uwanja wa Stamford Bridge.

Comments