John Terry anongeza mwaka Chelsea


Beki wa kati anayekipiga katika timu ya Chelsea John Terry amesaini mwaka mmoja baada ya mashabiki wa timu hiyo kumwomba aendelee kubaki.

John Terry 35, aliongea na mashabaki wa timu hiyo katika mechi ya mwisho dhidi ya Leicester city ambao wengi walimtaka nahodha huyo abaki kwa mwaka mwingine.

Terry alichipukia katika timu ya West Ham 1991-95, na kuibukia katika timu ya vijana mwaka 1995-98 na kuingia rasmi katika timu ya wakubwa kwenye mwaka 1998 hadi sasa.

Terry amecheza idadi ya mechi zisizopungua 703 hadi sasa na ameingia kwenye historia ya mashujaa ya timu hiyo yenye maskani yake jijini London.




Comments