Kane, Vardy waibeba England


Washambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Jamie Vardy na Harry Kane jana wameibeba timu yao ya taifa baada ya kila mmoja kufunga goli dhidi ya Uturuki.

Kane alianza kuipatia England bao dakika 3 ya mchezo ambapo kwenye dakika ya 13 Hakan Calhanoglu wa Uturuki aliweza kuchomoa bao hilo kwenye dakika ya 13.

Kipindi cha pili Kocha wa Uingereza alibadilisha taswira ya mchezo baada ya kuwatoa Raheem Sterling na Jack wilshere baada ya nafasi zao kuchukuliwa na Danny Drinkwater pamoja Jordan Henderson.

Licha ya Kane kukosa penati lakini juhudi binafsi za mchezaji Jamie Vardy ziliinua matumaini ya ushindi kwa Uingereza baada ya kutupia bao la ushindi kwenye dakika ya 83 ya mchezo na matokeo kubaki 2-1 hadi mwisho.

Comments