Kessy asaini miaka 2 Yanga


Beki wa kulia anayekipiga katika timu ya Simba Hassan Kessy atavaa rasmi uzi Yanga baada ya kusaini dili la miaka 2 la kuichezea timu hiyo kuanzia mwezi ujao.

Kessy amefikia uamuzi kwa kuwa Simba haikuweka mkataba mwingine mezani ili kumalizana nae na hivyo Yanga ndiyo timu pekee iliyofikia makubaliano ya kumalizana na mchezaji huyo ambaye amemaliza mkataba wake na Simba.

Zoezi la kusaini mkataba lilifanyika juzi jijini Dar es Salaam ambapo Kessy aliambatana na meneja wake Tippo Athumani kwenye hatua zote za kukamilisha dili hilo.

Simba sasa itabakiwa na beki Mnyarwanda Emery Nimuboma kwa upande wa kulia baada ya Kessy kusaini mkataba na Yanga.

Comments