Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa hana pressure katika mchezo wa fainali utakaochezwa leo dhidi ya Sevilla nchini Uswisi.
Katika mahojiano na waandishi wa habari Klopp alisema kuwa ana imani na vijana wake kuwa watarudi na ushindi, na kusisitiza ndio jambo pekee lilitawala vichwa vyao.
"Nina imani na wachezaji wangu bila shaka watacheza kwa ajili ya ushindi wa timu, matarajio yetu ni ushindi."
Klopp aliongeza kuwa kitendo cha wachezaji wake kujituma na kuingia fainali kimejenga furaha kwake. "Ata wachezaji walipoweza kuingia fainali limekuwa jambo la furaha kwangu" alisema
"Ni matumaini yetu tutapata mafanikio, tutajaribu kadri tuwezavyo lakini Sevilla anafikiria jambo hilo pia hapo ndo kwenye tatizo" Aliongeza Klopp
Liverpool inashuka dimbani kuchuana na Sevilla ambaye ndiye bingwa mtetezi wa kombe hilo, ikiwa ni nafasi yao pekee ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya 2016/17.

Comments
Post a Comment