Roy Hodgson alisema alikuwa akisubiri kukamilika kwa ratiba ya ligi kuu Uingereza (EPL) ili aweze kupata wachezaji sahihi watakoipeperusha bendera ya taifa hilo nchini Ufaransa.
Mipango ya kocha huyo iliingia dosari kutokana na mchezaji Danny Welbeck kupatwa na majeraha yatakayomweka nje wiki sita huku mchezaji mwenzake Oxlade Chamberlain naye atakosa fainali hizo kutokana na majeraha.
kocha huyo anatarajiwa kutangaza kikosi cha timu hiyo leo majira ya saa 5 asubuhi katika uwanja wa wembley nchini humo.

Comments
Post a Comment