Kocha wa Ufaransa anawaza nini kichwani mwake?


Baada ya timu ya taifa ya Ufaransa kupotea kwa muda kunako mchezo wa soka tangu mwaka 2006, kuna kila dalili huenda kikosi cha wachezaji bora kimeanza kurudi katika ardhi yao kama kile kizazi cha Zinedine Zidane na Thiery Henry.

Ukitoa safu ya ulinzi kuna neema ya viungo Ufaransa kuna N'golo Kante, Paul Pogba, Dimitri Payet, Lassana Diara, Blaise Matuidi, Yohan Cabaye, Hatem Ben Arfa, Frank Ribery na wengine wengi tunapata jibu huenda ufaransa imejaaliwa sasa.

Ingawa kila binadamu ana mapungufu lakini mapungufu mengine yako wazi. Ufaransa ina washambuliaji hatari kwa sasa tukianza na Karim Benzema, Alexander Lacazzete, Kevin Gameiro, Oliver Giroud, Andre Pierre Gignac na Cedric Bakambu.

Ingawa Ufaransa ni mwenyeji wa mashindano lakini binafsi sioni nafasi ya Ufaransa kuchukua kombe la Euro mwaka huu, ingawa sijui Didier Deschamps ambaye ni kocha wa Ufaransa anawaza nini lakini binafsi napata majibu kuwa Ufaransa haiwezi kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Binafsi sioni nafasi ya Andre Pierre Gignac katika kikosi cha Ufaransa, simuhesabu katika ulimwengu wa soka ikiwa kuna Alexandre Lacazzete wa Olympic Lyon na Kevin Gameiro wa Sevilla ambao wana makali, nguv, spidi na uwezo mkubwa wa kufumania nyavu kuliko Gignac.

Ikiwa Lacazzate ndiye mfaransa pekee ambaye angalau alimpa changamoto mfungaji bora wa PSG Zlatan Ibrahimovic leo hii kocha anamwacha anamchukua Andre Pierre Gignac na Oliver Giroud ambao wote wana mpira wa aina moja.

Bila shaka hakuna anayepinga uwezo wa Antonio Griezmann wa Atletico Madrid, kasi na uwezo wake vinamfanya kuwa mchezaji pale Calderon akifunga katika kila mechi muhimu anaenda kucheza na Andre Pierre Gignac pamoja na Oliver Giroud hivi ni vituko na ubaguzi wa wazi katika hadhi ya kiwango.

Ingawa Cedric Bakambu hana uzoefu na michuano ya kimataifa lakini ni mshambuliaji bora katika timu ya Villareal. Uwezo wa Kevin Gameiro ni mkubwa kwa sasa kulinganisha na ule wa Oliver Giroud na Gignac lakini anamwacha na kubeba magarasa.

Mpira wa leo umetawaliwa na kasi na mfumo wa 4-3-3 ambao unahitaji washambuliaji wenye kasi zaidi, Lacazzete anafiti katika mfumo huo, kama timu ina Pobga, Matuidi, kante au Payet katika sehemu ya kiungo nadhani kuna washambuliaji wenye kasi wanahitajika zaidi.

Wakati fulani mashindano huwa ni magumu zaidi unahitaji wachezaji wenye kasi na wasumbufu kwenye Ngome pinzani aina ya wachezaji kama Ben Arfa na Frank Ribery wanahitajika katika kuipa nguvu fowadi yenye kasi, huwez kumkosa Karim Benzema, Lacazzete au Kevin Gameiro kwa sababu ni wazi Oliver Giroud na Andre Gignac hawawezi kubeba majukumu hayo.

Binafsi sikufikiria uwepo wa kiungo Yohan Cabaye, Moussa Sissoko na Andre Pierre Gignac wala kukosekana kwa Alexande Lacazzete, Karim Benzema na Kevin Gameiro ndiyo maana nikasema sijui kocha wa Ufaransa anawaza nini kichwani mwake kuhusiana na kikosi alichonacho kulinganiswa na michuano hiyo.

Binafsi ndoto za Ufaransa kutwaa ubingwa huo kama Ubelgiji, Ujermani, Hispani zitavuka hatua ya nusu fainali.
 

Comments