Liverpool yasajili golikipa


Timu ya Liverpool jana imekamilisha usajili wa aliyekuwa mlinda lango wa timu ya Mainz ya nchini Ujermani Loris Karius.

Liverpool ilikamilisha taratibu za vipimo vya mchezaji huyo jana na sasa anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na liverpool baada ya kumwaga wino kwa dau la euro 4.7 milioni.

Jurgen Klopp alikuwa akitafuta golikipa mzuri wa kutoa changamoto kwa golikipa namba moja wa timu ya Liverpool Simon Mignolet na sasa klopp amefanikiwa baada ya kukamilisha dili la kipa huyo mwenye miaka 22.

Comments