Lukaku: naondoka Everton


Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku amesema kuwa anataka kuondoka Goodson park ili kuinua zaidi jina lake kwenye ulimwengu wa soka.

Lukaku 23, ana miaka 3 tangu ajiunge na miamba ya hiyo ya Liverpool akitokea chelsea na katika muda wote amekuwa moja kati ya washambuliaji bora katika ligi ya EPL.

Lukaku alisisitiza kuwa licha ya kuwa na msimu mzuri Everton lakini anaona huu ni wakati sahihi wa kuachana na Everton ili kujiunga na timu kubwa zaidi barani Ulaya.

"Pamoja na kuwa nimekuwa kwenye kiwango bora hapa everton, lakini ni muhimu pia kwangu kuondoka na kutengeneza jina langu kwenye ulimwengu wa soka." Alisema Lukaku

Huenda Lukaku amefikia uamuzi baada ya kuona baadhi ya timu zenye majina makubwa barani Ulaya zikimtolea macho ikiwemo Juventus na PSG.

Comments