Man united yamwondoa LvG


Timu ya Manchester united imevunja mkataba rasmi na Luus van Gaal na sasa siyo kocha wa timu hiyo tena.

Manchester united ilificha mpango wa kumwondoa kocha huyo kabla ambao ulikuwepo hata kabla ya kuchezwa kwa fainali za kombe la FA dhidi ya Crystal Palace.

Pamoja na kupewa fungu la kutosha la usajili msimu uliopita lakini LvG alishindwa kuipa mafanikio timu hiyo baada ya kukaa kwa miaka 2 Old Trafford

Kuondoka kwa kocha huyo kutazuia baadhi ya nyota kuachana na timu kama ilivyokuwa kwa De Gea ambaye alisema wazi asingebaki endapo Van Gaal angeendelea kuwa kocha wa timu hiyo.

Timu hiyo itakabidhiwa kwa kocha Mreno Jose Mourinho siku chache zijazo baada ya kukamilika kwa mpango wa dili hilo.

Comments