mayanja: Yanga imepatia kumsajili Juma Mahadh


Kocha wa timu ya Simba Jackson Mayanja amesema kuwa Yanga imelamba dume baada ya kukamilisha usajili wa kiungo wa Coastal Union Juma Mahadh.

Mahadh amesaini mkataba wa miaka 3 Yanga na Mayanja anaamini mchezaji huyo ni jembe kwa kuwa aliwahi kumfundisha kabla hajatua Simba.

"Nadhani Yanga imeoata mchezaji mzuri atawasaidia katika msimu ujao kwani ana uwezo mkubwa wa kutoa changamoto kwa viungo wengine kikosini." Alisema

Juma Mahadh alionesha kiwango kikubwa msimu katika timu yake msimu huu kiasi cha kumshawishi kocha Bonifasi Mkwasa kumwita kwenye timu ya taifa.

Comments