Mourinho amwaga wino Man united


Timu ya Manchester united imekata mzizi wa fitna baada ya kumpa Jose Mourinho mkataba wa miaka mitatu.

Mreno huyo ambaye amewahi kuinoa Fc Porto, Chelsea, Intermilan na Real Madrid ndiye kocha rasmi wa Manchesetr united baada ya kukamilika kwa dili hilo.

"Ni heshima ya pekee kuwa kocha wa Manchester united, hii ni timu kubwa duniani na watu wengi wanaipenda." Alisema Mourinho.

Mourinho ataelekea nchini Ureno kufanya mazungumzo na wanachuo siku ya jumatatu na jumanne na hivyo mashabiki wa Manchester united wataweza kumuona siku ya jumapili.

Comments