Mourinho kuanza na Ibrahimovic


Kocha Jose Mourinho ameweka mipango kwa kuanza na mchkato wa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic.

Mourinho sasa ana uhakika na kibarua cha Old Trafford baada ya kuwepo kwa uvumi wa timu kumwondoa rasmi kocha wa sasa Louis van Gaal.

Kuondoka kwa Ryan Giggs ni dalili kuwa Mourinho yupo njian kutua Manchester united kwa kuwa Giggs aliweka wazi hawezi kufanya kazi na Mourinho.

Mourinho atakabidhiwa dau la euro 200 milioni ili kufanya usajili wa kuirudisha Manchester uinted kwenye kinyang'anyiro cha ubingwa na tayari ameweka mpango wa kumsajili Ibrahimovic ambaye aliwahi kumfundisha alipokuwa na Intermilan

Comments