Kocha anayetarajiwa kutua Manchester united Jose Mourinho amesema anavutiwa na mpango wa kumleta Willian Old Trafford.
Mourinho anataka kuweka mezani ofa ya dau la euro 60 milioni ili kufanikisha mpango wa kumsajili nyota huyo ambaye alikuwa anafanya vizuri alipokuwa nae Chelsea.
Mourinho anaamini Willian ni moja ya mchezaji aliyekuwa anajitoa wakati akiinoa Chelsea na ndio maana anavutika na mpango kumleta Old Trafford.
Jose Mourinho anatarajiwa kusaini mkataba wake na Manchester united siku ya ijumaa baada ya kufanya makubaliano binafsi na viongozi wa timu hiyo.

Comments
Post a Comment