Mourinho kutua man uinted


Timu ya Manchester united inajiandaa kufanya mazungumzo na Jose Mourinho ili achukue nafasi ya Louis van Gaal.

Hatua hiyo imekuja baada ya kocha aliyepo sasa kwenye timu hiyo kuchemsha kuchukua ubingwa licha ya kupewa fungu zito la usajili katika kipindi cha majira ya joto.

Licha ya Van Gaal kutumia dau la euro 250 milioni lakini ameshindwa kupeleka ubingwa Old Trafford kama alivyoahidi na mbaya zaidi amekosa nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Nyota kadhaa akiwemo kipa wa Man united David De Gea alisema kuwa hawezi kubaki kwenye timu hiyo kama LvG ataendelea kuwa kocha jambo linaloisukuma Manchester kuharakisha kutua kwa Jose mourinho kwenye timu hiyo.

Manchester united itafanya mazungumzo na Jose Mourinho wiki ijayo ili kufanya makubaliano mbalimbali.

Comments