Mchezaji wa timu ya West Ham united Mark Noble amesema kwa sasa hafikirii kuichezea timu ya taifa ya Uingereza hadi kocha aliyepo sasa atakapo ondoka kwenye timu hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kocha wa Uingereza Roy Hodgson kumuacha kiungo huyo na kuwachukua Danny Drinkwater wa Leicester city na Fabian Delph wa Manchester city ambao atawatumia kwenye nafasi ya kiungo.
Noble ambaye pia ni nahodha wa West Ham alisema kuwa hana chuki na wachezaji hao lakini hadhani kama viungo hao walikuwa bora kuliko yeye msimu huu.
"Nilikua na msimu mzuri lakini nimeumia kuyakosa mashindano, sina ubaya na Drinkwater wala Delph lakini nimekuwa kwenye kiwango bora kuliko wao." Alisema Noble
"Nimeamua kustaafu timu ya taifa mpaka pale Roy atakapoachana na timu ya taifa, nawatakia mafanikio katika safari ya ufaransa. Sitaangalia mechi nitakua ibiza" Aliongeza mchezaji huyo.

Comments
Post a Comment