Timu ya Yanga imeweka wazi kuwa inajiandaa kumuongezea mkataba mpya kocha wao Hans Pluijm anayemaliza mkataba wake hivi karibuni.
Yanga inafanya vizuri chini ya Pluijm ikiwa ni pamoja na kuchukua ubingwa wa ligi kuu mara mbili mfululizo na kuingia kwenye hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Licha ya mpango wa kumuongeza mkataba kocha huyo Yanga imepania kuimalisha zaidi benchi lake la ufundi ikiwa kwenye mipango ya kumuongeza mkataba mpya kocha makipa wa timu hiyo Juma Pondamali.

Comments
Post a Comment