Ranieri kuongeza nguvu kwa Yannick Bolasie


Huenda kocha wa timu ya Leicester city Claudio Ranieri anataka kuongeza zaidi kwenye timu yake baada ya kutenga dau lenye thamani ya euro 40 milion ili kuwanasa Yannick Bolasie wa Crystal palace na mshambuliaji Troy Deeney wa Watford.

Ranieri amefikia uamuzi huo ili kuinua timu yake ambayo itakua na kibarua cha kutetea ubingwa wa EPL pamoja na kufanya vizuri katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Gazeti la nchini Uingereza limeeleza kuwa tayari kocha uyo yupo kwenye mipango ya kuwanasa wachezaji hao ambao wanafanya vizuri kwenye timu zao.

Yannick Bolasie na Troy Deeney ambaye ni nahodha katika timu ya Watford wamekuwa kwenye kiwango bora msimu huu jambo pekee linalomvutia Ranieri kuwasajili wachezaji hao.

Comments