Rashford aweka rekodi England


Mshambuliaji kinda wa Manchester united Marcus Rashford ameweka rekodi kwenye timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kijana zaidi kufunga kwenye mechi ya kwanza.

Rashford 18, aliichezea Uingereza kwa mara kwanza ambapo kwenye  dakika ya 9 ya mchezo alizamisha bao wavuni katika mechi dhidi ya Australia.

Pia ameingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kinda kuwahi kufunga kwenye timu hiyo baada ya Michael Owen na Wayne Rooney.

Comments