Ripoti ya mayanja kuwaondoa wageni Simba, yaumia kichwa na pengo la Majabvi


Kocha wa Simba Jackson Mayanja juzi aliwasilisha ripoti yake inayoonesha mabadiliko ndani ya kikosi Simba kwa kamati ya Ufundi ya timu hiyo.

Katika ripoti hiyo Mayanja aliweka wazi nia yake juu ya kuondolewa kwa wachezaji wa kigeni akiwemo Juko Mursheed, Hamis Kiiza, Paul Kiongera, Bryan Majegwa na Paul Kiongera kutokana na viwango duni na ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya wachezaji.

Ripoti ya kocha huyo pia imependekeza kuachwa kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Mohamed Fakhi na Hassan Isihaka na kuitaka kamati hiyo itoe ridhaa juu ya kutolewa kwa mkopo kwa Said Ndemla ili aongeze kiwango zaidi.

Pia ripoti imebainisha kuwa kipa namba moja wa timu hiyo Vicent Angban anatakiwa kubaki kkutokana na kiwango bora alichoonesha na kiwango cha hali ya juu hata hivyo Justice Majabvi ameitaka radhi timu hiyo imwache aungane na mkewe aliyehamishiwa kikazi nchini Australia.

Licha ya kuwa na mgongano kwenye suala la ndemla kutolewa kwa mkopo bado Simba ipo kwenye wakati mgumu wa kumpata mbadala wa kiungo Justice Majabvi ambaye ameweka wazi kuwa ataungana na mkewe nchini Australia.


Comments