Mchezaji nyota wa Real Madrid Christiano Ronaldo amesema licha ya kuwa Jose Mourinho atairudisha hadhi ya Manchester united lakini hatajiunga nao.
Ronaldo ana imani kuwa Man united wanaweza kurudisha hadhi ya jina lao kupitia kocha huyo lakini haoni sababu itakayomrudisha Old Trafford kwa sasa.
Ronaldo 31, aliongeza kuwa haoni timu nyingine kwa sasa itakayompa furaha zaidi ya Real Madrid na hivyo ana imani atakaa zaidi katika timu hiyo,
"Jose ni kocha mzuri lakini sina sababu ya kurudi Man united, nina furaha na maisha ya Madrid nipo kwenye timu bora na hapa ndipo mahali pekee nipatapo furaha." Alisema Ronaldo

Comments
Post a Comment