Rooney kuanzia benchi England


Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amesema kuwa mshambulaji na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza huenda akaanzia benchi katika timu yake.

Hodgson amesema kuwa hakuna dhamana ya moja kwa moja kwa Wayne Rooney huenda akaanzia benchi mbele ya Harry Kane na jamie Vardy.

Kocha huyo ameongeza kuwa Harry Kane na Jamie Vardy wamefunga jumla ya magoli 49 msimu huu hivyo ni wazi kuwa wako kwenye kiwango bora kuliko nahodha huyo.

Hata hivyo Hodgson alisema kuwa atamwangalia Rooney katika mechi za majaribio dhidi ya Uturuki na Australia na kumtumia upande wa kushoto katika mfumo wake 4-3-3 ili kuweza nafasi sahihi ya kumtumia mshambuliaji huyo.

"Rooney ni mchezaji mzuri na anajituma uwanjani, sote tunajua mambo makubwa aliyofanya na ni msaada wetu kwenye michuano iliyo mbele yetu, lakini nitamwangalia zaidi katika mechi tatu za majaribio." Alisema kocha huyo.

Comments