sevilla yainyuka liverpool 3-1, yabeba kombe la europa mara ya 3.


Timu ya Sevilla imezima ndoto za Liverpool kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kuinyuka timu hiyo mabao 3-1 katika mchezo wa fainali.

Liverpool ilipata bao la kuongoza kupitia Daniel Sturridge  ambalo lilidumu hadi kipindi cha mapumziko lakini kipindi cha pili Sevilla ilichoma goli hilo na kuongeza mengine mawili kupitia Kevin Gameiro, na Coke ambaye alifunga mabao mawili yaliyobaki.

Kwa  ushindi huo Sevilla sasa inaandika rekodi ya kutwaa taji hilo mara mfululizo baada ya kunyakua taji hilo mwaka 2014 dhidi ya Benifica, 2015 dhidi ya Dnipro ya Ukraine na jana dhidi ya Liverpool.

Liverpool haitashiriki michuano yoyote ya mabingwa Ulaya msimu wa 2016/17 baada ya kukosa taji hilo na kukosa nafasi tatu za juu ili kushiriki europa ligi baada ya zile nne zinazopeleka wale watakaoshiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Comments