Simba kusajili wanne kimataifa


Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Zacharia Hanspoppe amesema kuwa timu hiyo inajipanga kusajili nyota wa nguvu ambao wana viwango bora na wenye hadhi ya kimataifa.

Hanspoppe alisema kuwa mbali na kusajili pamoja na kusuka upya kikosi hicho kwa kusajili nyota wenye viwango vya juu kimataifa, vilevile wameadhimi kuwarudisha baadhi ya wachezaji walipanda viwango ambao walitolewa kwa mkopo kwenye timu zingine.

"Tumeadhimia kuwarudisha nyota wetu ambao tuliwatoa kwa mkopo na wanafanya vizuri katika zingine, tayari tumekwisha andaa orodha ya wachezaji hao." alisema Hanspoppe

Hata hivyo mwenyekiti huyo hakuweka wazi ni nyota gani wenye hadhi ya kimataifa wameadhimia kuwasijili kwa ajili ya kusuka upya timu hiyo.  

Comments