Simba kusajili wazoefu


Timu ya Simba sasa imefanya makubaliano ya kusajili wachezaji wenye majina makubwa kuliko kutumia zaidi vijana wanaochipukia katika timu yao.

Uamuzi huo umekuja baada ya timu hiyo kushindwa kubeba ubingwa wa ligi kuu kwa miaka minne sasa na hali inayoonesha kuwa huenda timu ikaporomoka.

Katika kipindi cha miaka minne Simba imeshindwa kushiriki michuano ya kimataifa kutokana na kukosa nafasi mbili za juu katika msimamo wa ligi na kupelekea uongozi wa timu hiyo kuchukua uamuzi huo rasmi.

Kuna kila dalili huenda Simba ikaachana na wachezaji wake wa kigeni na kubaki na goli kipa Vicent Angban pekee ambaye nidye anaonekana ana nafasi kubwa ya kubaki.

Comments