Uongozi wa timu ya Simba umeweka wazi kuwa wanataka kuachana na mpango wa kusajili wachezaji kutoka Kenya na Uganda.
Simba inataka kukimbilia Afrika magharibi katika nchi za Ghana, Ivory Coast na kwingineko kusaka nyota bora zaidi ili kusuka kikosi chao.
Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya wachezaji walisojiliwa kutoka kenya na Uganda kuwa mizigo kwenye timu yao.
Simba imeweka wazi kuwa ni Juuko Murshed na Emmanuel Okwi pekee ndio waliofanya vizuri kwenye timu baada ya wengine kuchemsha akiwemo Paul Kiongela na Danny Serrunkuma.
Hata hivyo Simba iliwasifu golikipa Vicent Angban kutokana Ivory Coast na Mzimbabwe Justice Majabvi ambao wamefanya vizuri kwenye timu yao.

Comments
Post a Comment