Uongozi wa timu ya Simba sasa upo kwenye mchakato wa kutafuta kocha makini atakayeiwezesha timu yao kufanya vizuri msimu ujao.
Simba imekuwa ikifanya mchakato wa kupata makini wa kigeni lakini haijaweka wazi mchakato huo ambao umekuwa ukifanyika kimya kimya.
"Ni kwel tupo kwenye harakati za kupata kocha mpya, tunahitaji kocha mzuri ili timu yetu iweze kufanya vizuri msimu ujao." Kilisema chanzo
Habari za chinichini zinasema moja kati ya wa wageni wanaofukuzia dili hilo ni kocha aliyeipa Simba ubingwa mara ya mwisho mwaka 2012 Milovan Cirkovich ambaye inasadikika ameshatuma maombi yake Simba.

Comments
Post a Comment