Sturridge arejea mazoezini


Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge sasa atajumishwa kwenye kikosi cha Roy Hogdson baada kurejea mazoezini.

Daniel Sturridge alikosa mechi ya kirafiki dhidi ya Australia kutokana na jeraha la goti lakini sasa yuko fiti na kocha wa England Roy Hogdson atamjuisha mchezaji kukamilisha kikosi cha wachezaji 23.

Hodgson atatangaza tena kikosi chake atakachotimka nacho kuelekea Ufaransa hadi kufikia jumanne na wachezaji wawili wataungana na Fabian Delph nje ya kikosi.

Comments