Yanga kupokewa kesho alasiri


Timu ya Yanga inatarajiwa kuwasili kesho majira ya katika uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere ikitokea nchini Angola.

Yanga inasubiriwa kwa hamu na msululu wa mashabiki ambao watafika kuwapokea kesho baada kutua uwanjani hapo.

Mashabiki wana hamu ya kuipongeza timu hiyo ambayo imefuzu hatua ya makundi baada ya kuichomoa Esperansa ya Angola kwa idadi ya magoli 2-1 baada ya kuchezwa kwa mechi ya nyumbani na ugenini.

Yanga itapokea kiasi kisichopungua milioni 800 za kitanzania ikiwa ni pesa ya maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na hatua ya makundi.

Comments