Yanga kuweka kambi Uturuki


Timu ya Yanga inajiandaa kuweka kambi nchini Uturuki ili kujiandaa na hatua makundi kwenye michuano ya kombe la shirikisho.

Kamati ya mashindano ya timu hiyo imeriadhia mpango huo baada ya kikao kilichofanyika juzi ambacho kilimuhusisha kocha mkuu wa timu hiyo Hans Der Pluijm.

Yanga imepanga kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kukabiliana na timu ya Aljeria MO Bejaia Juni 17 Mwaka huu.

Aidha timu hiyo itatoa mapumziko ya siku tano kwa wachezaji ambao hawakuitwa kwenye timu za taifa na wataungana na wenzao kwenye kambi hiyo baada ya majukumu mazito ya kutumikia taifa lao.

Comments