Yanga noma sana, yaipasua Azam 3-1 fainali


Timu ya Yanga imedhihirisha kuwa haishikiki msimu huu baada ya kuichapa Azam kipigo cha mabao 3-1 katika fainali ya kombe la FA.

Katika mchezo huo mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe alifunga magoli mawili dakika ya 9 na 47 ya mchezo na bao la tatu lilifungwa na Deus Kaseke kwenye dakika ya 81 ya mchezo huku bao pekee la Azam likifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Didier Kavumbagu.

Yanga imekusanya mataji yote ya ligi ya nyumbani ikiwemo lile la Vodacom na hili la shirikisho na sasa imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kujipanga kwenye hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Yanga imekuwa ikifanya vizuri tangu kutua kwa kocha Hans Pluijm na kuzipiku Simba na Azam kwa ubora.

Comments