Yanga yawaongeza mkataba wachezaji wake


Timu ya Yanga imewaongeza imetoa mikataba mipya kwa wachezaji wake wazawa ambao ambao mikataba yao ilikuwa imefika ukingoni.

Yanga iewapa mkataba wa miaka miwili wachezake wake akiwemo Oscra Joshua, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Ally Mustafa 'Barthez', na Juma Abdul ambao kwa pamoja mkataba wao utafikia kikomo ifikapo mwaka 2019.

Yanga imefanikiwa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho hivyo imepanga kujiimarisha zaidi ili kuwa na kikosi imara zaidi kwenye michuano hiyo.

Yanga imeweka wazi kuwa haitaacha mchezaji wake yeyote mzawa msimu huu na hivyo wamekamilisha zoezi hilo kwa kuwaongeza mkataba wachezaji wake.

Comments