Timu ya Al-Ahly ya Misri inavutika na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma.
Ngoma ambaye aliiweka Al-Ahly ya Misri kwenye wakati mgumu baada ya kuchomoa bao safi la kichwa katika mchezo wa marudiano alisema yupo tayari kupokea ofa hiyo.
"Al-Ahly ni timu kubwa siwezi kukataa ofa hiyo endapo itakuja" alisema Ngoma
Ngoma aliyetokea Platinum ya Zimbabwe amekuwa kwenye kiwango bora tangu atue Yanga na kufanya vizuri katika ligi ya ndani na michauno ya kimataifa Afrika na hadi sasa amefunga jumla ya mabao 17 huku mabao 3 akifunga kwenye michuano ya mabingwa Afrika.

Comments
Post a Comment