Vicent alisema kuwa licha ya kuwapo na ushindani mkubwa wa namba kwenye timu hiyo lakini atapambana ili kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha mwalimu Hans Pluijm.
"Najua kuna ushindani mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga lakini nitapambana ili niweze kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza." Alisema Andrew
Yanga inajiimarisha zaidi katika safu ya ulinzi kutokana na kupata mechi nyingi ndani ya ligi na za michuano ya kimataifa na huenda Andrew Vicent akaisaidia katika nafasi ya Kiungo wa kukaba ambapo timu hiyo haijapata mchezaji rasmi wa namba hiyo
Comments
Post a Comment