Timu ya Arsenal inajipanga kukamilisha usajili pacha wa wachezaji wa Leicester city Jamie Vardy pamoja Riyad Mahrez.
Arsenal imefikia pazuri na Jamie Vardy lakini sasa wanajipanga tena kumnasa na Mahrez ambaye ndiye mchezaji bora wa ligi England msimu huu.
Huenda Arsenal ikaweka mezani dau la euro 20 milioni kama lile la Vardy ili kumnasa Mahrez ambaye alinunuliwa kwa dau la euro 400000 milioni kutoka Le Havre ya Ufaransa.
Vardy na Mahrez kwa pamoja walifunga magoli 41 kwenye ligi ya EPL msimu huu, Vardy alitikisa nyavu mara 24 huku Riyad Mahrez akiwa amefunga magoli 17.

Comments
Post a Comment