Baada ya kumkosa mshambuliaji wa Timu ya Leicester city Jamie Vardy Arsenal sasa yahamishia usajili kwa Islam Sliman wa Lisbon.
Vardy 29 alikubali dili ya la miaka minne Leiester na kuvunja rasmi matumaini ya Arsenal kwa mshambuliaji huyo na sasa timu hiyo inaona mshambuliji wa Algeria ndiye suluhisho.
Lisbon iliweka kipengele cha dau la euro 24 milion kama ada ya uhamisho kwa timu itakayohitaji kumsajili Sliman 28, anayefanya vizuri katika ligi ya Ureno.
Arsenal inajipanga kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo aliyefunga jumla ya goli 27 msimu uliopita kwenye ligi ya Ureno.

Comments
Post a Comment