Azam yaachana na Ivo Mapunda


Timu ya Azam FC imeamua kuachana na kipa Ivo Mapunda na sasa imejikita kwenye  mpango mpya wa kusajili kipa mwingine.

Ivo alisajiliwa na Azam baada ya kunyimwa mkataba mpya na timu ya Simba ambapo Azam iliamua kumchukua na kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

Hata hivyo Azam iliamua imeamua kuachana na kipa huyo kutokana na kutoridhishwa na kiwango alichoonesha tangu ajiunge na wana ramba ramba hao.

"Tumeamua kuachana na Ivo Mapunda na sasa tupo kwenye mipango ya kusajili Kipa mwingine" kilisema chanzo.

Comments