Timu ya Barcelona imeungana na timu ya PSG ya ufaransa katika mbio za kumwania Phelippe Coutinho wa Liverpool.
Mabingwa hao wa Spain wanataka kuongeza nguvu kwenye kikosi chao na wanaona Coutinho ni mchezaji muhimu wa kurithi nafasi za kina Adres Iniesta pale Catalunya.
PSG ilitenga dau la awali la euro 30 milioni ili kuishawishi Liverpool kumtoa mchezaji huyo ambaye amekuwa nguzo tangu atue Anfield akitokea Intermilan.
PSG inatakiwa iongeze nguvu kumsajili Coutinho huenda Barca ikawa na ushawishi mkubwa wa kumnasa nyota huyo wa Liverpool kutokana na urafiki mkubwa kati yake na nyota wa Barcelona Neymar.

Comments
Post a Comment