Timu ya Barcelona imehamia kwenye zoezi la kumsajili beki wa Manchester united Daley Blind ambaye ana maisha ya mashaka tangu kutua kwa Jose Mourinho,
Barcelona imefikia uamuzi huo baada ya Javier Mascherano kuweka wazi kuwa atatimka kwenye timu hiyo na kuelekea Juventus.
Timu ya Barcelona inakadiriwa kutenga dau la euro 14 milion ili kufanikisha usajili wa Daley Blind licha ya Mourinho kumuweka sokoni kwa dau la euro 18 milioni.
Daley Blind na Juan Mata hawaoni sababu ya kubaki united kutokana na ujio wa Mourinho kwenye timu hiyo ni wazi hawatakuwa chaguo lake hali inayosadikika huenda Barcelona ikakamilisha dili hilo mapema.

Comments
Post a Comment