Timu ya Newcastle itashuka dimbani katika ufunguzi wa ligi ya Championship nchini England katika uwanja wa Craven Cottage dhidi ya Fulham Agosti 5 mwaka huu.
Ratiba ya ligi daraja la kwanza imetoka leo baada ya kutangulia ile ya ligi kuu ya England (EPL) na Agosti 5 ligi hiyo itaanza rasmi.
Newcastle chini ya kocha Rafael Benitez inaanza upya harakati zake za kupambana ili kurejea EPL baada ya kushuka daraja.
Benitez anafungua ukurasa mpya na timu ya Newcastle baada ya kuchemsha akiwa na Napoli pamoja na Real Madrid na sasa kocha huyo wa zamani wa Liverpool ana kibarua kizito cha kuirejesha timu hiyo ligi kuu.

Comments
Post a Comment