Bonucci akubali kutua Chelsea


Kocha mpya wa Chelsea Antonio Conte huenda akakamilisha dili la kumsajili beki kitasa anayekipiga kwenye timu ya Juventus Leonardo Bonucci baada ya kukubali ofa ya Chelsea.

Cont ambaye kwa sasa anamalizana na timu ya taifa ya Italy anataka kumuongeza kumuongeza mkataba mlinzi huyo wa kati baada ya kuumia mara kwa mara kwa beki ya kati ya Chelsea Kurt Zouma na John terry.

Zouma bado anasumbuliwa na majeraha ambayo yatamweka muda mrefu nje uwanja jambo linalomsukuma kocha huyo kumsajili mlinzi wake wa zamani wa Juventus na sasa kwenye timu ya taifa.

Bonucci amekubali kupokea ofa ya Chelsea kutokana na kuwa na ukaribu na kocha huyo ambaye aliwahi kumfundisha alipokuwa Juventus.

Comments