Licha ya Simba kuamua kuachana kabisa na Haruna Chanongo lakini timu ya Stand imempa mkataba wa miaka miwili mchezaji huyo.
Habari zilizagaa kuwa Stand united ilimtema mchezaji huyo jambo ambalo limekanushwa na katibu mkuu wa Stand united Dk Jonas Tiboroha.
Dk Tiboroha alisema kuwa habari zilizozagaa kuhusiana na timu hiyo kuachana na Haruna Chanongo si za kweli na tayari wamempa mkataba wa miaka 2 mchezaji huyo.
"Taarifa zilizozagaa kuhusiana na kuachana na Chanongo si za kweli, bado ni mchezaji wetu na tayari ameshasaini miaka miwili ya kuitumika timu yetu." Alisema Dk Tiboroha.

Comments
Post a Comment