Timu ya chelsea imeanza kufikiria mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke kama itamkosa Romelu Lukaku wa Everton.
Lukaku anafukuziwa na PSG huenda akafuta mpango wa kurudi katika timu yake ya zamani Chelsea na kutua kwa mabingwa hao wa Ufaransa ambao mshambuaji amekua chaguo lao namba moja.
Kutokana na upinzani mkubwa wa kumsajili Lukaku unaooneshwa na PSG huenda Chelsea ikaachana na Lukaku na kumsajili Benteke licha ya kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Juventus ya Italy.
Liverpool imeshindwa kumtumia mshambuliaji huyo aliyefunga goli 9 katika mechi 29 alizocheza na huenda ikamweka sokoni kufidia dau lao usajili la euro 32 milioni.

Comments
Post a Comment