City yamtaka Bravo wa Barcelona


Timu ya Manchester city inavutika na mpango wa kumsajili kipa wa Barcelona Claudio Bravo kama mbadala wa Joe Hart.

Manchester city haivutiwi na kiwango cha kipa namba moja wa timu hiyo Joe Hart ambaye amechemsha pia kwenye michuano ya UEFA Euro baada ya kucheza chini ya kiwango.

Pep Gurdiola anataka kufanya marekibisho kadhaa ili kujenga upya kikosi hicho chini ya mfumo wake na sehemu ya golikipa inaonekana kutomridhisha kocha huyo.

Endapo City itafanikiwa kumnasa Claudio Bravo 33, huenda golikipa huyo wa England akapoteza namba moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha timu kutokana na kiwango bora alichonacho kipa huyo wa Barcelona.

Comments