Courtois aiwaza Euro sasa


Golikipa namba wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Thibaut Courtois amesema sasa akili yake inawaza michuano ya EUFA euro licha ya klabu yake kufanya vibaya EPL.

Courtois 24, alisema kuwa chelsea ilishindwa kupata kombe lolote msimu ulioisha lakini ana imani watarekebisha makosa yao msimu ujao.

Courtois aliongeza kuwa kwa sasa ndoto yake ni kuhakikisha anaisaidia timu yake ya Ubelgiji kutwaa ubingwa wa kombe Euro nchini Ufaransa.

"Timu yetu ni nzuri na tuna kikosi chenye nguvu matarajio yetu ni kufika fainali ili tuweze kutwaa taji hilo." Alisema kipa huyo.

Comments