Coutinho kuwatoa PSG mamilioni


Timu ya PSG inaanda mpango kambambe wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool Phelippe Coutinho kwa dau la euro 45 milioni.

PSG ambao ni mabingwa mara tano mfululizo wa ligi ya Ufaransa inataka kumsajili nyota huyo wa Liverpool ikiwa ni sehemu pekee ya kujaza nafasi itakayoachwa na Zlatan Ibrahimovic.

Ibrahimovic ameweka wazi huenda akatimka Paris na kuanza maisha mpya ya soka kwenye timu nyingine baada ya kufanya mambo makubwa akiwa na PSG kwa miaka minne sasa.

 Liverpool inaingia kwenye wakati mgumu wa kumlinda kiungo huyo ambaye amekuwa akizitoa udenda timu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Barcelona na Real Madrid.

Comments